Bi’idhnillah, Timu ya "Zainabiyya Foundation" (ZF) imefanikiwa kusambaza Meli za Maji katika maeneo ya Gaza ambako Wanaume, Wanawake, na Watoto wamekuwa wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa Maji Safi ya kunywa.
Waumini hao watukufu waliochangia katika mpango huu wameshiriki katika kukata kiu ya wadhulumiwa wa Ghaza, ikiwa ni sehemu ya kukumbuka kwa moyo wa dhati kabisa kiu isiyovumiliwa iliyo wapata Familia Tukufu ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika Ardhi ya Karbala, Siku ya A'shura. Familia ya Mtume (s.a.w.w) waliouwa na kufa Kishahidi huku wakiwa na kiu kali imewabana.
Mwenyezi Mungu aikubali ibada hii na awanyanyue daraja ya juu wale wote waliounga mkono msaada huu wa kukata kiu cha wadhulumiwa wa Ghaza.
Timu ya ZF.
Your Comment